Seventh-Day Adventist Church

BOKO ADVENTIST CHURCH

Menu

TUCASA EXCELLENT

TUCASSA EXCELLENT walio chini ya Kanisa la Waadventista Boko ndani ya mtaa wa Tegeta wanaendesha mahubiri ya hadhara yakiandamana na huduma za afya ambapo watu hupimwa na kupewa dawa na ushauri wa kidaktari na wataalamu kutoka chuoa cha utabibu Excellent. Jumamosi iliyopita ya 15/09/2019 kulifanyika ubatizo wa kwanza ambapo watu 123 walibatizwa. Imeelezwa kuwa hii ni idadi ya juu kuwahi kubatizwa katika eneo hilo. Ubatizo mwingine unatarajiwa kufanyika juma lijalo.Mungu aibariki kazi yake na vijana wa TUCASA waliojitolea kuwahudumia watu kiroho na kimwili.

Taarifa ya ziada ni kuwa baada ya ubatizo wa kwanza wa watu 123 uliofanywa na mchungaji Robert Matekere kwenye mto Simiyu, ubatizo mwingine wa watu 85 umefanyika Jumamosi ya tarehe 21/09/2019 na Mchungaji Robert Matekere na hivyo kufanya idadi ya wote waliobatizwa kwenye mkutano huo wa injili wa majuma matatu kufikia 208. Mungu apewe sifa kwa mafanikio hayo.