Siku ya Jumamosi ya tarehe 30/01/2021, ilikuwa Sabato ya pekee wakati Mhazini wa Jimbo la Union Mission ya Kusini mwa Tanzania Athanas January Sigoma alipowekewa mikono ya uchungaji kwenye Kanisa la waadventista wa Sabato Morogoro Mjini. Sigoma alifanyiwa huduma hiyo pamoja na wachungaji wenzake ambao kabla ya kuwekewa mikono walikuwa wakihudumu kama wachungaji wa mitaa. Wachungaji wengine waliowekewa mikono ni Fredrick Kibaso Nyankonda wa mtaa wa Jamaika, Mmbara Peter Mumbara wa mtaa wa Mazimbu, Nathanael Joseph Kipangule wa mtaa wa Zanzibar, na Baraka Sadock Butoke wa mtaa wa Magomeni.
Washiriki wa Boko - mahali anaposalia Athanas Sigoma na familia yake -- walikuwepo kumpongeza kwa hatua hiyo ya ushindi. Mungu ambariki Athanas Sigoma kwa utumishi huo mpya.

Washiriki wa Boko - mahali anaposalia Athanas Sigoma na familia yake -- walikuwepo kumpongeza kwa hatua hiyo ya ushindi. Mungu ambariki Athanas Sigoma kwa utumishi huo mpya.