Tarehe 15/09/2019 ilifanyika Sabato maalumu ya ujirani mwema ambapo wageni wengi walialikwa kuja kuabudu na waumini wa Kanisa la Waadventista Boko. Miongoni mwa walioalikwa ni kikundi cha uimbaji cha Ellen Singers, na The Voice. Pamoja na vikundi vya uimbaji, wengine walioalikwa na kikundi cha Changamoto ni Matumaini kinacholea walioamua kuachana na madawa ya kulevya. Huduma ya siku hiyo iliendeshwa na Petro Muganda - mchungaji wa mtaa wa Mwenge, Aston Mmamba - mchungaji wa Shirika la habari la Kanisa la Waadventista Tanzania, Athans Sigoma - Mhazini wa Union ya Kusini, na Stephen Letta - mchungaji wa mtaa wa Tegeta. Hapa chini ni baadhi ya picha zikionesha matukio ya siku hiyo.












